Jihad Taha, msemaji wa harakati hiyo ya mapambano ya Palestina amesema Jihad Islami inaunga mkono mawazo na mapendekezo yote ambayo yatafanikisha haraka kufikiwa mapatano ya kusimamisha vita.
Amesema, Jihad Islami inawatolea wito wapatanishi wote kumfahamisha Trump kuhusu duru zilizopita za mazungumzo na nafasi ya Netanyahu katika kuzuia jitihada za kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Wakati huo huo gazeti la Kizayuni la Maariv limefichua kuwa Steven Witkoff, Mjumbe Maalumu wa White House katika Masuala ya Mashariki ya Kati jana aliwasilisha mpango mpya kwa ajili ya mapatano ya kubadilishana mateka wakati alipokutana na kuzungumza na viongozi wa kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, mpango ambao unaweza kuifanya Hamas kulegeza misimamo na hivyo kuanda njia kwa ajili ya usitishaji vita wa kudumu katika Ukanda wa Gaza.
Maariv limeandika kuwa: Kulingana na vyanzo viwili vikuu vya Israel, Wamarekani hawaoni tena mpango wa awali wa Witkoff kama ufunguo wa kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa hiyo wamependekeza ufumbuzi mpya.
342/
Your Comment